Karibu kwenye Meza ya Magazeti, ambapo tunakuletea kile kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti mbalimbali nchini Tanzania leo Jumatano, Desemba 03, 2025.
ZANZIBAR LEO
Kichwa Kikuu:
DK. SAMIA: WATANZANIA TUSITUMIKE KUIHUJUMU NCHI
- Rais Samia atoa rai kwa wananchi kuongeza umakini na kutokubali kutumiwa kuhatarisha amani ya taifa.
- Dk. Mwinyi aweka msisitizo katika kilele cha siku ya watu wenye ulemavu.
MWANA SPOTI
Kichwa Kikuu:
DIARRA ASHTUA
- Kiungo wa Simba agusa rekodi za CAF, aendelea kutajwa kwenye namba za kimataifa.
- Pantev afichua jambo, bosi wa Simba atoa kauli.
- EPL leo: Arsenal vs Brentford saa 4:30 usiku.
UELEKEO
Kichwa Kikuu:
DK. SAMIA AONYA VURUGU, ASEMA TANZANIA HAIWEZI KUAMRISHWA
- Rais atoa tahadhari dhidi ya makundi yanayojaribu kuhatarisha amani ya nchi.
- Wazee wa Dar es Salaam wafunguka walivyofadhaishwa na vurugu za Oktoba 29.
- Ofisa Magereza akamatwa akidaiwa kuhusika kwenye tukio la mauaji ya mwenzi wake.
























Hakuna maoni:
Chapisha Maoni