Karibu kwenye Meza Yetu ya Magazeti ya leo Ijumaa, Desemba 05, 2025, tukikuletea kwa ufupi taarifa zote kubwa zilizopewa kipaumbele na magazeti makubwa nchini. Endelea hapa kupata muhtasari kamili wa stori za siasa, michezo, uchumi na matukio mbalimbali yanayoendelea Tanzania.
đź“° MWANASPOTI
WHY MATOLA
Wadau wa soka wamempongeza kocha Matola na kutaka apewe timu, huku yeye mwenyewe akifunguka kuhusu mustakabali wake ndani ya Simba.
PACOME, DUBE WAIZIMA FOUNTAIN
Yanga yaendelea kutamba baada ya ushindi wa 2–0 dhidi ya Fountain Gate.
EPL: ASTON VILLA vs ARSENAL
Kesho Jumamosi, saa 9:30 usiku, Villa Park – mtanange mzito kusubiriwa.
BOXING DAY – 26/12
Mapambano makubwa ya masumbwi yatarajiwa kufanyika Boxing Day mwaka huu.
đź“° UHURU
VIJANA LINDENI AMANI – DKT. MIGIRO
Dkt. Asha Migiro atoa wito kwa vijana kuhakikisha amani inatunzwa na kukataa kushiriki vurugu.
RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO WA IPU
Rais Samia ahutubia mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani, akitangaza msimamo wa Tanzania kwenye masuala ya kimataifa.
MABALOZI WA EU WAKUTANA NA SPIKA ZUNGU
Mazungumzo yamelenga kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya.
WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA KUANZA MASOMO KWA MKUPUO
Serikali yatangaza kuanza rasmi kwa mfumo wa masomo ya kidato cha kwanza kwa mpangilio maalumu.
đź“° HABARILEO
SERIKALI: TUENZI AMANI TUSIGEUKE WAKIMBIZI
Waziri Simbachawene asisitiza umuhimu wa amani, akionya kuwa vurugu hazijawahi kuisaidia nchi yoyote.
DK MIGIRO: TAIFA LINDWE, TUJIVUNIE UMOJA
Atoa wito kwa Watanzania kudumisha ustahimilivu na mshikamano.
937,581 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2026
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2026 yatangazwa rasmi.
MRADI WA HEET KUONGEZA UBORA MUHAS
Serikali yatoa zaidi ya bilioni 120 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu ya juu.




















Hakuna maoni:
Chapisha Maoni