Breaking


Jumamosi, 27 Desemba 2025

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20, MAFURIKO KUTOKEA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini-TMA, imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo katika mikoa 20 hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA, leo imetaja mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani.

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia kesho, Jumapili, na huenda zikasababisha madhara ikiwemo mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Hivyo, wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa hususan walioko mabondeni na maeneo hatarishi, wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

Aidha, TMA imewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

Hakuna maoni: