Breaking

Ijumaa, 19 Desemba 2025

SIMBA SC WAMKARIBISHA RASMI KOCHA MKUU MPYA, STEVE BARKER


Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha safu yake ya benchi la ufundi baada ya kumtambulisha rasmi Kocha Mkuu mpya, Steve Barker, hatua inayotarajiwa kuipa timu msukumo mpya kuelekea mafanikio makubwa zaidi ndani na nje ya nchi.


Kupitia taarifa yake rasmi, Simba SC imemtaka Barker kama sehemu ya mkakati wa klabu kuijenga timu imara, yenye ushindani mkubwa katika mashindano ya ndani pamoja na michuano ya kimataifa. Ujio wa kocha huyo unatajwa kuwa ni sehemu ya dhamira ya uongozi wa klabu kuhakikisha Simba inaendelea kuwa miongoni mwa vigogo wa soka barani Afrika.


Steve Barker anakuja na uzoefu mkubwa katika soka la ushindani, akiwa amewahi kuzinoa klabu mbalimbali na kuonesha uwezo mkubwa wa kuibua vipaji, kuimarisha nidhamu ya kikosi pamoja na kusimamia falsafa ya soka la kisasa linalozingatia ushindani na matokeo chanya. Mashabiki wa Simba SC wanatarajia kuona mabadiliko chanya katika mbinu za uchezaji, maandalizi ya kikosi na matokeo ya jumla ya timu chini ya uongozi wake.


Uongozi wa Simba SC umeeleza kuwa una imani kubwa na uwezo wa kocha huyo mpya, huku ukisisitiza kuwa Barker atapewa ushirikiano wa kutosha ili kutimiza malengo yaliyowekwa na klabu kwa msimu huu na misimu ijayo. Mashabiki, wanachama na wadau wa soka wametakiwa kumpa kocha huyo sapoti ya kutosha ili kufanikisha safari mpya ya mafanikio.


Hakuna maoni: