Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inaendelea kujifua kuelekea mchezo wa kwanza kwenye Mashindano ya AFCON 2025 dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria mjini Sale, Rabat nchini Morocco.
Kikosi kinaendelea kufanya mazoezi yakilenga kuimarisha mbinu za kiufundi na utimamu wa mwili.
Taifa Stars itafanya mazoezi ya mwisho kwenye mji mwingine wa Fes uliopo umbali wa takribani kilomita 202 kutoka Rabat, kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho na kuzoea mazingira ya uwanja utakaotumika katika mchezo huo.
Mchezo kati ya Tanzania na Nigeria unatarajiwa kuchezwa tarehe 23 Desemba 2025 katika mji wa Fes.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni