Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, tarehe 23 Desemba 2025.
Kwa ujumla, mikoa mingi nchini inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi na ngurumo katika maeneo machache, huku vipindi vya jua vikijitokeza mara kwa mara.
Mikoa inayotarajiwa kupata mvua na ngurumo katika maeneo machache ni pamoja na Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Kigoma, Tabora, Katavi na ukanda wa Ziwa Victoria.
Kwa mikoa ya Kati, Mashariki, Kaskazini, Kusini Mashariki, Pwani pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, kunatarajiwa mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
📌 Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa rasmi kutoka TMA kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni