Breaking


Jumatano, 24 Desemba 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa angalizo kwa wananchi, hususan wakazi wa Mkoa wa Ruvuma, kuchukua tahadhari kutokana na vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika maeneo machache ndani ya saa 24 zijazo. Wananchi wanashauriwa kuzingatia tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, ikiwemo mafuriko ya ghafla na usumbufu wa shughuli za kila siku.

Maeneo Yanayotarajiwa Kupata Hali ya Mawingu, Mvua na Ngurumo

Mikoa ya Dodoma na Singida

Kusini mwa Mkoa wa Morogoro

Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu

Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma


Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.


Mikoa ya Lindi na Mtwara

Inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi,

Mvua katika maeneo machache,

Pamoja na vipindi vya jua.


Maeneo ya Pwani na Kaskazini Mashariki

Visiwa vya Unguja na Pemba

Mikoa ya Tanga na Dar es Salaam

Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro

Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara

Mkoa wa Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia)


Maeneo haya yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.


TMA inaendelea kusisitiza wananchi kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuchukua tahadhari zinazostahili, hususan katika maeneo yenye uwezekano wa mvua kubwa kwa vipindi vifupi.

Hakuna maoni: