Breaking

Alhamisi, 18 Desemba 2025

WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI WASIOPELEKA MICHANGO NSSF KUCHULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano,  Deus Sangu, amewaagiza viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waajiri wa sekta binafsi wanaoshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinawanyima wafanyakazi haki zao za msingi ikiwemo mafao ya uzeeni.

Sangu alitoa maelekezo hayo tarehe 17 Desemba 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za NSSF jijini Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kwanza NSSF tangu alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika ziara hiyo, aliambatana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Rahma Kisuo. Ambapo amesema kuwa ni wajibu wa kisheria kwa kila mwajiri wa sekta binafsi kujiandikisha katika Mfuko, kuwaandikisha wafanyakazi wake na kuwasilisha michango yao kwa wakati kila mwezi, hivyo Serikali haitavumilia uzembe au makusudi ya kukiuka sheria kwa waajiri wanaohatarisha mustakabali wa wafanyakazi wao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, amesema mafanikio haya yametokana na jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya ajira na uwekezaji pamoja na mikakati ya Mfuko kuwafikia waajiri wa sekta binafsi na wananchi waliojiajiri pamoja na kuboresha mifumo ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha huduma za Mfuko kwa waajiri, wanachama na wadau kwa ujumla.






Aidha  Sangu ameipongeza NSSF kwa kuongezeka thamani Mfuko kufikia itrilioni 10, kutoka trilioni 4.8 mwaka 2021. 

Hakuna maoni: