Kampuni ya ya Airtel Tanzania imewataka wanavyuo nchini kutumia fursa ya kimtandao katika kuwasaidia kuboresha taaluma zao pindi wawapo vyuoni.
Hayo yamebainisha na Meneja wa Airtel Staff Saccos, Gasper Swai, katika hafla fupi katika Chuo Cha biashara (CBE) kilichopo jijini dar es salaam, ambapo amesema lengo kuu la hafla hiyo ni kuwakutanisha vijana pamoja ili kuweza kuwasaidia kufanikisha malengo yao pindi wawapo vyuoni.
Aidha, Gasper amesema kuwa mitandao imekuwa ikitoa wigo mpana katika kuwasaidia wanafunzi katika kutafuta taarifa mbalimbali za kimasomo hivyo uwepo wa huduma za kimtandao za Airtel kupitia bidhaa mbalimbali zikiwemo 5g Router au Pocket Wifi kutasaidia kuongeza vijana wenye chachu ya matumizi ya teknolojia nchini.
Hata hivyo katika hatua nyingine, Gasper amesema kutokana na uhitaji wa huduma ya kimtandao vyuoni lengo la hafla hii si kuhitimisha katika chuo cha biashara (CBE) pekee bali ni mwanzo mzuri wa kuvifikia vyuo vyote vya hapa nchini katika kuhakikisha Inatoa fursa sawa kwa vijana wote nchini.
Kwa upande wake Joakim Faustine ambaye ni Waziri wa Sanaa na utamaduni, katika chuo cha biashara(CBE) amesema ujio wa kampuni ya Simu ya Airtel chuoni hapo si kutoa burudani tu bali ni pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi itakayowasaidia kutambua vitu vya kufanya na ambavyo si vya kufanya ili kuwasaidia kufanikisha malengo yao pindi wawapo chuoni hapo.
Sambamba na hilo Joakim ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwasaidia vijana nchini kupitia ajira katika sekta mbalimbali hapa nchini huku akiwaaasa vijana kitambua wanachohitaji pindi wawapo vyuoni.
Nae, Mwanafunzi wa Chuoni hapo Twaha Kalulu amewataka wanafunzi wenzake kuzingatia masomo pindi wawapo vyuoni pamoja na kuachana na vitendo visivyofaa katika jamii vitakavyoweza kupelekea kukatisha masomo Yao.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni