Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Mick Kiliba ameongoza kikao kazi cha Mafunzo kwa wasimamizi wa usaili - Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 14 Disemba, 2025 katika Ukumbi wa Karimjee.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika kila mkoa Nchini yakiwa na lengo la kuwakumbusha wasimamizi wa usaili kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za uendeshaji wa mchakato wa ajira ili kuhakikisha HAKI inatendeka na wasailiwa wanapata kazi kulingana na uwezo na umahiri waliouonyesha katika saili hizo.
“Mwanzoni mwa mwezi wa kumi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi ya kuajiri nafasi 12,000 za kazi ndani ya siku 100 za kwanza baada ya kuapishwa, ambapo nafasi 5000 ni kwa kada za Afya na nafasi 7000 kwa kada za Elimu. Sekretarieti ya Ajira ilishaanza kazi ya kutekeleza Maagizo hayo na leo hii nyinyi mmeteuliwa kuhakikisha adhma ya Mhe. Rais inatekelezwa kwa wakati ili kabla ya siku 100 kufika tuwe tumekamilisha kupata wataalamu wenye si



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni