WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo 08 Januari 2026, anazungumza na Wamachinga pamoja na madereva wa pikipiki na bajaji za kubeba abiria katika kongamano la mwaka linafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limewakutanisha wadau wakuu wa sekta ya wamachinga na usafirishaji wa pikipiki na bajaji, kwa lengo la kujadili na kutafakari mustakabali wa sekta hizi katika mchango wake kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa Taifa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni