Mahakama Kuu ya Guinea imethibitisha ushindi wa Koloneli Mamady Doumbouya katika uchaguzi wa rais uliofanyika Desemba 28, na hivyo kufungua njia kwake kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa miaka saba baada ya kupata asilimia 86.72 ya kura. Uchaguzi huo ulifanyika katika kipindi cha mpito chini ya utawala wa kijeshi, kufuatia shinikizo kutoka ECOWAS na jumuiya ya kimataifa kurejesha utawala wa kiraia.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulikumbwa na utata mkubwa, huku vyama vya upinzani vikisusia na baadhi ya wagombea kupinga uhalali wake. Mshindi wa pili, Abdoulaye Yero Baldé, ambaye awali alipinga matokeo, baadaye aliondoa shauri lake mahakamani. Wakosoaji, akiwemo rais wa zamani Alpha Condé aliyeko uhamishoni, waliukosoa mchakato huo wakidai haukuwa huru wala wa haki.
Baada ya uamuzi wa mahakama, Doumbouya alitoa wito wa umoja wa kitaifa, wakati mjadala ukiendelea kuhusu mustakabali wa demokrasia nchini Guinea chini ya utawala wa kijeshi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni