Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Joseph Daudi Mwakalinga, maarufu kwa jina la mtandaoni @jiggerman, mkazi wa Zimbili, Kinyerezi, Wilaya ya Ilala, kwa tuhuma za kumjeruhi mtoto wake (jina limehifadhiwa).
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 08, 2026, katika eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam. Mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio hilo katika mazingira yanayoendelea kuchunguzwa na vyombo vya usalama.
Jeshi la Polisi limesema kuwa hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kushirikisha mamlaka nyingine husika, huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
Aidha, Polisi Dar es Salaam imetoa wito kwa wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kujiepusha na vitendo vyote vya ukatili, hususan dhidi ya watoto, na kuzingatia sheria na misingi ya ulinzi wa mtoto.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni