NEMC Kanda ya Morogoro Rufiji imeshiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Lameck Mwigulu Nchemba iliyowataka wawekezaji na watanzania kuzingatia masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi wakati wa utekelezaji wa miradi au kilimo ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.
Ameyasema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi wa mafuriko katika Mkoa wa Morogoro na kukuagua makazi na mashamba ya wananchi wa Kilosa, kidete, miundombinu ya Reli ya SGR na MGR, pamoja na kutoa pole na hifadhi ya muda kwa Kaya 140 zenye idadi ya watu 506 Katika maeneo ya shule ya msingi Tindiga, Kijiji Cha Tindinga kilichopo Kata ya Tindiga.
Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu alielekeza mambo makuu ya kuchukua hatua ambayo ni Ujenzi wa Mabwawa ya zamani yaliyobomoka, pamoja na bwawa kubwa la kuvunia maji, kaguzi katika miundombinu hasa ya barabara na madaraja kwa wakati, uzingatiaji wa masuala ya Mazingira ikiwa ni pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza athari za mafuriko, Watu kutokujenga mabondeni au kwenye mikondo ya maji
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu aliambatana na viongozi wengine wa Serikali wakiwemo: Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo na Waziri wa Fedha Mhe. Khamis Mussa Omari Pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo John Dugange.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni