Breaking


Jumamosi, 17 Januari 2026

REA YASAINI MIKATABA YA TRILIONI 1.2 YA KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI 9,009

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesaini mikataba 30 yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vitongoji 9,009 utakaonufaisha Wateja wa awali 290,300  katika mikoa 25 ya Tanzania Bara.

Akizungumza katika hafla hiyo leo, Januari 17, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kusaini kwa mikataba ya Mradi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha ifikapo 2030 vitongoji vyote nchini viwe vimefikishiwa nishati ya umeme.

“Serikali imedhamiria kuhakikisha hakuna Mtanzania atakayebaki bila umeme. Tumekamilisha vijijini na sasa ni zamu ya vitongoji na kwa mikataba hii iliyosainiwa hivi leo ni ushahidi wa dhamira hiyo ya Serikali,” amesema Mhe. Ndejembi.

Amebainisha kuwa kati ya mikataba 30 iliyosainiwa, mikataba 21 ni ya kampuni za Wazawa na mikataba mingine tisa ni ya kampuni kutoka Nje ya nchi ambazo zimesajiliwa hapa nchini.

Serikali ya Rais Samia inatambua Sekta ya Nishati ni injini ya kuchochea maendeleo na amekuwa akitoa fedha nyingi ili kuboresha maisha ya Wananchi wa vijijini.

Ameipongeza REA kwa kuendelea kuwa chombo imara cha Serikali kwa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya kusimamia na kupeleka nishati bora kwa Wananchi na ameendelea kuhakikisha kuwa Taasisi zote za Umma ziunganishwe na umeme zikiwemo shule za msingi, sekondari na vituo vya afya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali itaendelea na kasi yake ya kusambaza umeme ili kuleta tija inayokusudiwa.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu amepongeza jitihada za REA katika kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha nishati ya umeme inasambaa kote nchini.

"Hongereni REA mnafanya kazi kubwa, leo hii tumefurahi kushuhudia tukio la kihistoria.


Hakuna maoni: