Breaking


Ijumaa, 30 Januari 2026

SERIKALI YAIMARISHA ULINZI WA BINADAMU DHIDI YA WANYAPORI WAKALI



Serikali imeweka kipaumbele katika kuimarisha  ulinzi wa maisha ya wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu ikiwa ni mkakati wa kitaifa wa kusimamia utatuzi wa migongano baina ya binadamu na Wanyamapori. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  Mbunge wa Handeni Mhe. Charles Jacob Sungura (Mb), aliyetaka kufahamu kuwa, Serikali ina mkakati gani wa kutatua changamoto ya tembo wanaoharibu mazao na kuhatarisha maisha maeneo ya Mzeli, Sindeni na Kwamatuku

”Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Kuweka kituo cha kudumu cha Askari Wanyamapori katika eneo la Handeni kwa ajili ya mwitikio wa haraka kwenye matukio na kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu, kuimarisha doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu, kuendelea kutumia teknolojia za kisasa katika kudhibiti wanyamapori wakali na matumizi ya ndege nyuki (Drones) sambamba na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu rafiki za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu” Mhe. Chande

Mhe. Chande ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali imeanza kuandaa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya uzio wa umeme wa jua na teknolojia zinazofanana kwa lengo la kuweka utaratibu mzuri wa kujenga miundombinu ambapo tayari imeonesha ufanisi mkubwa katika nchi kadhaa barani Afrika  na hapa nchini katika mpaka wa Jumuiya ya Wanyamapori ya Ikorongo na vijiji vinavyopakana na eneo hilo 

Hakuna maoni: