Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kujadili na kuweka mikakati thabiti ya kuongeza ufanisi katika kutoa huduma bora kwa walipa kodi.
Akizungumza katika mkutano wa tathmini ya nusu mwaka unaoendelea jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema taasisi hiyo imeweka mkazo katika kusikiliza changamoto za walipakodi, kuboresha mifumo ya utoaji huduma, pamoja na kuongeza ufanisi kwa watumishi wake.
Amesema huduma bora kwa walipakodi si hiari bali ni wajibu wa msingi wa TRA, kwani ndiyo njia ya kujenga imani kwa wananchi na kuwahamasisha kulipa kodi kwa hiari.
Mkutano huo unalenga kupitia utendaji wa kipindi cha Julai hadi Desemba 2025 na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi huduma kwa nusu mwaka inayofuata.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni