Breaking


Alhamisi, 8 Januari 2026

TRA YAWEKA MIKAKATI YA KUDHIBITI UKWEPAJI KODI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea na kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa nusu ya kwanza ya mwaka, kinachowakutanisha viongozi wake kutoka mikoa yote nchini, kinachofanyika jijini Arusha.

Kikao hicho kinajadili kwa kina mikakati ya kukabiliana na ukwepaji kodi, pamoja na kuweka mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya TRA katika miezi sita ijayo, kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato na uadilifu wa mfumo wa kodi nchini.

Viongozi wa TRA wanatarajiwa kubadilishana uzoefu, kutathmini changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao, na kuweka mikakati madhubuti itakayoongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa walipakodi na kuchangia maendeleo ya taifa.

Hakuna maoni: