Breaking


Alhamisi, 8 Januari 2026

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

 


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, tarehe 08 Januari 2026.


Kwa mujibu wa TMA, hali ya mawingu kiasi ikifuatwa na mvua na ngurumo inatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro pamoja na mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.


Mikoa ya Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua, hali inayofanana na inayotarajiwa katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.


Kwa upande wa mikoa ya Mara, Simiyu, Arusha, Manyara na Kilimanjaro, hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua inatarajiwa kutawala.


TMA imeonya kuhusu vipindi vifupi vya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 katika baadhi ya maeneo ya pwani ya kaskazini na kusini mwa Bahari ya Hindi, hususan mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.


Hakuna maoni: