Mamlaka ya hali ya hewa imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, tarehe 05 Januari 2026, huku ikitoa angazo muhimu kwa wakazi na wasafiri wa maeneo ya pwani.
⚠️ Angalizo la Hali ya Hewa
Vipindi vifupi vya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa, pamoja na mawimbi makubwa yanayoweza kufikia urefu wa mita 2, vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni pamoja na mikoa ya:
- Tanga
- Dar es Salaam
- Pwani (ikiwemo Visuwa vya Mafia)
- Lindi
- Mtwara
Pia, hali hii inatarajiwa kuonekana katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Wananchi, hususan wavuvi, wasafiri wa baharini na wakazi wa maeneo ya pwani, wanashauriwa kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni