Breaking


Jumapili, 11 Januari 2026

WAZIRI MASAUNI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO JIPYA LA ABIRIA BANDARI YA MKOANI, PEMBA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria katika Bandari ya Mkoani, iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba.


Akizungumza mara baada ya hafla hiyo, Waziri Masauni alisema mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu ya usafiri wa majini, kuboresha huduma kwa wasafiri pamoja na kuongeza ufanisi wa shughuli za bandari. Alibainisha kuwa ujenzi wa jengo hilo utasaidia kuongeza usalama, faraja na hadhi ya bandari hiyo muhimu kwa uchumi wa Pemba na Zanzibar kwa ujumla.


Waziri Masauni pia alisisitiza umuhimu wa miradi ya maendeleo kuzingatia uhifadhi wa mazingira, akieleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafuata viwango na taratibu za mazingira ili kuhakikisha maendeleo yanaenda sambamba na ulinzi wa mazingira.

Ujenzi wa jengo hilo jipya la abiria unatarajiwa kuboresha huduma za bandari, kuongeza uwezo wa kuhudumia abiria wengi zaidi na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Kusini Pemba.


Hakuna maoni: