Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Rhimo Simeon Nyansaho, tarehe 20 amefanya ziara katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ( MMUT), Kikombo pamoja na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Jeshi Msalato, Jijini Dodoma.
Waziri Nyansaho alianza kwa kutembelea MMUT ambapo alipokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman.
Akiwa MMUT, Waziri Nyansaho ametembelea ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo na kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi huo wa ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2020.
Baada ya kumaliza ziara yake MMUT, Waziri Nyansaho alielekea katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Kijeshi iliyoko Msalato ambapo pia alipata wasaa wa kuona ni kwa namna gani mradi huo umefikia katika hatua nzuri.
Waziri Nyansaho, amefurahishwa na ujenzi wa Hospitali hiyo ya Jeshi na amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Hospitali yenye uwezo wa kutoa huduma nzuri na za kiwango cha juu za matibabu hasa katika Jiji la Dodoma na hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutahakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya Jijini Dodoma
Waziri huyo amemaliza ziara yake huku akilipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa hatua iliyofikiwa katika miradi hiyo miwili.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni