Breaking


Alhamisi, 5 Februari 2026

VIDEO: BANTU RIDE YAINGIA SOKONI: SULUHISHO JIPYA LA CHANGAMOTO ZA USAFIRI WA KILA SIKU DAR ES SALAAM

Kwa wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam, usafiri wa kila siku umeendelea kuwa chanzo cha malalamiko yasiyoisha. Gharama zisizotabirika, uhaba wa madereva katika nyakati muhimu, pamoja na malalamiko ya makato makubwa kwa madereva wa majukwaa ya usafiri wa mtandaoni, vimeifanya sekta hii kuwa na maswali mengi kuliko majibu.

Kadri mahitaji ya huduma za usafiri wa kidijitali yanavyozidi kuongezeka, mjadala mkubwa umeibuka kuhusu nani anayenufaika zaidi na mifumo iliyopo abiria au watoa huduma.

Ni katika mazingira hayo ambapo huduma mpya ya usafiri wa kidijitali, Bantu Ride, imeingia rasmi sokoni, ikilenga kujipenyeza katika sekta inayokua kwa kasi lakini inayokabiliwa na changamoto za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza Februari 4 wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bantu Ride, Peter Msanga, alisema kuwa kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni sehemu ya juhudi za kutumia teknolojia kutatua changamoto halisi za usafiri zinazowakabili Watanzania kila siku.

“Leo tunazindua rasmi Bantu Ride, huduma ya usafiri wa kidijitali iliyojengwa kwa ajili ya Watanzania. Ni jukwaa la ndani linaloelewa mazingira yetu, changamoto zetu na mahitaji ya wasafiri wa kila siku,” alisema Msanga.

Hakuna maoni: