Breaking


Jumanne, 24 Februari 2026

BENKI KUU YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI FEBRUARI 24, 2026

 



Bank of Tanzania (BoT) imetoa viwango elekezi vya ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa tarehe 24 Februari 2026, vikionyesha mwenendo wa soko la fedha pamoja na bei ya dhahabu katika soko la kimataifa.



Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa Shilingi 2,555.4455 na kuuzwa kwa Shilingi 2,581. Aidha, Pauni ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa Shilingi 3,447.296 na kuuzwa kwa Shilingi 3,481.769, wakati Euro (EUR) inanunuliwa kwa Shilingi 3,011.0815 na kuuzwa kwa Shilingi 3,041.1923.


Kwa sarafu za Asia, Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa Shilingi 369.8559 na kuuzwa kwa Shilingi 373.5545. Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa Shilingi 16.4985 na kuuzwa kwa Shilingi 16.6634.


Katika ukanda wa Afrika, Rand ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa Shilingi 159.502 na kuuzwa kwa Shilingi 161.097. Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa Shilingi 19.7943 na kuuzwa kwa Shilingi 19.9923, huku Faranga ya Rwanda (RWF) ikiwa inanunuliwa kwa Shilingi 1.7477 na kuuzwa kwa Shilingi 1.7651. Kwa upande wa Uganda (UGX), kiwango cha ununuzi ni Shilingi 0.7104 na uuzaji ni Shilingi 0.7175, wakati Faranga ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa Shilingi 0.8609 na kuuzwa kwa Shilingi 0.8695.


Wakati huo huo, bei ya dhahabu imeelezwa kuwa Shilingi 13,193,100.93 kwa ununuzi na Shilingi 13,325,031.94 kwa uuzaji kwa kila wakia moja (Troy Ounce).


BoT imesisitiza kuwa viwango hivi ni vya maelekezo (indicative rates) na vinaweza kutofautiana kidogo kulingana na taasisi ya fedha au benki husika. 


Kwa taarifa zaidi, wananchi wanaweza kutembelea tovuti rasmi ya Benki Kuu ya Tanzania kupitia www.bot.go.tz au kufuatilia mitandao yake ya kijamii @bankoftanzania.


Hakuna maoni: