Breaking


Jumatatu, 9 Februari 2026

DKT. NCHIMBI AZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUUNGANISHA ELIMU NA VIWANDA.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amezindua rasmi mpango wa ushirikiano kati ya taasisi za elimu na sekta ya viwanda, akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wake kwa vitendo.


Uzinduzi wa mpango huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, wakiwemo viongozi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi za umma na binafsi.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi Nchimbi ameielekeza Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyoitoa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.


Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya viwanda na taasisi za elimu ni jambo la lazima katika dunia ya sasa, akibainisha kuwa elimu inayotolewa inapaswa kumwandaa mwanafunzi kukabiliana na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda.


Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Elimu Wanu Hafidh, Naibu Katibu Mkuu wa CCM John Mongela, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.


Hakuna maoni: