Waziri wa Mawasiliano ya Habari, Angellah Kairuki, ameipongeza Kampuni ya Airtel Tanzania kwa uwekezaji wake unaolenga kuchochea ukuaji wa huduma za kidijitali nchini, akisema ni mchango mkubwa katika kuharakisha ajenda ya mageuzi ya teknolojia na mawasiliano.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa maduka 31 ya kisasa ya Airtel Smart Shops, Waziri Kairuki alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini.
Amesema kuwa uzinduzi wa maduka hayo ya kisasa unaonesha dhamira ya dhati ya Airtel Tanzania katika kuunga mkono matumizi ya teknolojia ya kisasa, huku ukiwapa wateja mazingira rafiki ya kupata huduma za mawasiliano, intaneti na suluhisho mbalimbali za kidijitali.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, uwekezaji huo unaendana na mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma bora za mawasiliano na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali unaokua kwa kasi.
Uzinduzi wa Airtel Smart Shops nchi nzima unatarajiwa kuongeza ufanisi wa huduma, kurahisisha upatikanaji wa teknolojia, pamoja na kuchangia kukuza ubunifu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni