Hapa katika eneo la Stendi ya Zamani Nzega mkoani Tabora, wananchi wamejitokeza kwa wingi kuwasilisha kero zao mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Kenan Kihongosi, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Wananchi hao wameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi, familia na mahitaji ya matibabu huku wakisisitiza matumaini yao ya kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Kihongosi amewahakikishia wananchi kuwa malalamiko yao yamesikilizwa na yatafanyiwa kazi kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za wilaya na mkoa. Amesema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza moja kwa moja sauti za wananchi na kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii, akisisitiza kuwa CCM itaendelea kusimamia utekelezaji wa ahadi zake kwa vitendo.
Ziara hiyo imeendelea kuwa jukwaa muhimu la mawasiliano kati ya viongozi na wananchi, ambapo maswali na maoni yalitolewa kwa uwazi na kujibiwa papo kwa papo. Wananchi wa Nzega wameonyesha imani yao kwa chama hicho, wakieleza kuwa ujio wa Kihongosi ni ishara ya kujali na kuthamini mchango wa wananchi katika maendeleo ya Taifa.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni