Breaking


Ijumaa, 6 Februari 2026

KIM KARDASHIAN AVUNJA UKIMYA: “UPENDO WA FAMILIA YETU UTAENDELEA” LICHA YA DRAMA ZA KANYE WEST


Malkia wa reality TV na mfanyabiashara maarufu, Kim Kardashian, ameweka mambo hadharani kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mume wake Kanye West, huku akisisitiza kuwa licha ya drama na changamoto zinazoendelea kumkumba Kanye, wao bado watabaki kuwa familia.

Akizungumza katika mahojiano na jarida la Complex, Kim mwenye umri wa miaka 45 alisema wazi kuwa msingi wa mahusiano yao baada ya talaka ni ushirikiano na maslahi ya watoto wao. Alieleza kuwa hakuna kinachoweza kubadilisha ukweli kwamba wao wameunganishwa milele kupitia familia.

“Sisi tutakuwa familia kila wakati na tutaendelea kushirikiana. Sote wawili tunajua hilo. Tutakuwa sawa, na kuna upendo mwingi kwa familia yetu. Tunataka kilicho bora kwa watoto wetu,” alisema Kim.

Kim Kardashian na Kanye West wana watoto wanne, na kwa mujibu wa Kim, ustawi wao ndiyo kipaumbele kikubwa kuliko tofauti zozote binafsi. Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Kanye amekuwa akikumbwa na mijadala na matukio yanayozua taswira hasi katika vyombo vya habari.

Kauli ya Kim imewavutia mashabiki wengi, wakimtaja kama mfano wa ukomavu, busara na uzazi wenye uwajibikaji, huku akionyesha kuwa hata baada ya ndoa kuvunjika, heshima na mshikamano kwa ajili ya watoto vinaweza kuendelea.

Kwa wengi, huu ni ujumbe mzito unaoonesha kuwa familia haimaliziki kwa talaka, bali hubadilika kwa namna ya kushirikiana kwa ajili ya mustakabali wa watoto.

Hakuna maoni: