Inaelezwa kuwa uhusiano kati ya rapa maarufu duniani Cardi B na staa wa mpira wa Marekani (NFL) Stefon Diggs umefikia tamati. Dalili kuu zinazochochea tetesi hizo ni hatua ya wawili hao kuacha kufuatana (unfollow) kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, jambo linalotafsiriwa na wengi kama ishara ya kuvunjika kwa mahusiano yao.
Licha ya Stefon Diggs kushiriki fainali ya Super Bowl, Cardi B hakuonekana wala kutoa kauli yoyote ya kumuunga mkono au kuzungumzia matokeo ya mchezo huo, hali iliyoongeza maswali miongoni mwa mashabiki wao.
Cardi B na Diggs walionekana pamoja kwa mara ya kwanza hadharani Novemba 2025, uhusiano uliopata gumzo kubwa mitandaoni. Inadaiwa mtoto aliyepatikana ni wa nne kwa Cardi B na wa tano kwa Diggs, ambaye kwa jumla anatajwa kuwa na watoto sita.
Gumzo zaidi yaliibuka baada ya kubainika kuwa Cardi B alipata ujauzito huo kabla ya kukamilika kwa talaka yake na aliyekuwa mume wake, Offset, jambo lililozua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii.
Hadi sasa, hakuna kati ya Cardi B wala Stefon Diggs aliyethibitisha rasmi taarifa za kuachana kwao, lakini ishara zilizopo zimeendelea kuwafanya mashabiki kuamini kuwa penzi hilo huenda limefikia mwisho. 👀

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni