Super Star wa muziki duniani, Chris Brown, amezungumza kuhusu uwezekano wa kuonekana kwenye Super Bowl Halftime Show, akithibitisha kuwa mashabiki wake wanataka kumuona akitumbuiza kwenye jukwaa hilo kubwa.
Kupitia Insta Story yake muda mfupi baada ya kumalizika show ya Super Bowl iliyofanywa na Bad Bunny, Chris Brown aliandika:
“Nadhani ni salama kusema wananihitaji mimi.” ✍
Tukio hili linakuja wiki kadhaa tu baada ya kampeni kuanzishwa na mashabiki, wasanii na wadau wa muziki, wakiwemo Ne-Yo na rapa Boosie Badazz, wakisisitiza kuwa Chris Brown anatakiwa kuonyesha kipaji chake kwenye hafla hiyo ya kimataifa.
Mashabiki wa Brown wameonyesha shauku kubwa kupitia mitandao ya kijamii, wakiweka alama za moyo, maoni na kutuma video za kumtia moyo msanii huyo, huku wakijaribu kuhakikisha jina lake linapewa nafasi kwenye show inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa michezo na muziki duniani.
Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa Super Bowl kuhusu msanii atakayekuwa sehemu ya show ijayo, jambo linaloongeza shauku na mijadala miongoni mwa mashabiki wa muziki.
Je, Chris Brown ndiye atakayepanda jukwaani mwaka huu? Mashabiki wanashindwa kuficha shauku yao, na tunasubiri kuona kama kampeni hii itafanikiwa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni