Breaking


Jumatano, 18 Februari 2026

MKUU WA MKOA WA RUKWA MHE. MAKONGORO NYERERE ATEMBELEA TASAC


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, leo tarehe 18 Februari, 2026, amefanya ziara katika Makao Makuu ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadilia maendeleo ya shughuli za usafiri wa majini katika mkoa wa Rukwa ambapo TASAC ina Ofisi za Kikanda.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum, Mhe. Nyerere ameipongeza TASAC kwa kuendelea Kudhibiti sekta ya usafiri majini katika mkoa wa Rukwa hivyo kupelekea watumiaji na shughuli zinazofanywa katika ziwa Rukwa kufanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu.

Mkuu wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya TASAC na Serikali za mikoa katika kuhakikisha kuwa watoa huduma wanazingatia viwango vya usalama na utunzaji wa mazingira. 

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Nyerere aligusia kuwa Mkoa wa Rukwa utakua mwenyeji wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ifikapo Oktoba 14, 2026.

Kwa upande wake, Bw. Salum alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kumtembelea na kuona utendaji kazi wa Shirika na kuahidi kuendelea kuongeza udhibiti katika Ziwa Rukwa ili kuepusha majanga yanayotokana na usafiri majini kwa wavuvi na watumiaji wengine wa ziwa hilo.

Bw. Salum aliongeza kuwa TASAC inaendelea kutekeleza mikakati yake madhubuti ya kuboresha huduma za usafiri kwa njia ya maji ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa salama na endelevu.

Mkurugenzi Mkuu alimuhakikisha Mkuu wa Mkoa kuwa TASAC itaendelea kushirikiana na mamlaka zote husika ili kuhakikisha usalama wa abiria na mizigo inayosafirishwa kwa njia ya maji.

Kikao hiko kilihudhuriwa na Mkurugenzi Huduma za Shirika, Bw. Hamid Mbegu pamoja na Meneja wa Uhusiano kwa Umma, Bw. Saidi Mkabakuli.

Hakuna maoni: