Breaking


Ijumaa, 6 Februari 2026

RAIS SAMIA AWATEUA DKT. KIDA NA DKT. MSEMWA KUWA MAKATIBU WAKUU OFISI YA RAIS - MIPANGO NA UWEKEZAJI



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, ambapo pia amewateua Makatibu Wakuu wawili katika Wizara hiyo.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia amemteua Dkt. Tausi Mbaga Kida kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango, pamoja na nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, huku Dkt. Fred Matola Msemwa akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Uwekezaji.

Taarifa ya mabadiliko hayo pamoja na uteuzi huo imetolewa leo, Februari 06, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Hakuna maoni: