Breaking


Ijumaa, 13 Februari 2026

SIKU YA RADIO DUNIANI


 Kila mwaka tarehe 13 Februari, dunia huadhimisha Siku ya Redio Duniani iliyoanzishwa na UNESCO na kuidhinishwa na United Nations. Mwaka 2026 maadhimisho haya yamebeba kauli mbiu ya “Radio and AI”, yakilenga kuangazia namna Akili Unde (AI) inavyoweza kuimarisha utendaji wa redio bila kupoteza mguso wa kibinadamu.

Redio ipo katika hatua mpya ya mabadiliko ambapo AI inaweza kusaidia kurahisisha kazi kama upangaji wa vipindi, taarifa za hali ya hewa na michezo, pamoja na uchambuzi wa wasikilizaji. Teknolojia hii pia inaweza kusaidia uhakiki wa taarifa (fact-checking) na kuboresha ubora wa maudhui, huku lengo kuu likiwa ni kulinda na kuimarisha imani ya wasikilizaji.

Hata hivyo, wataalamu wanasisitiza matumizi ya AI yawe ya kimaadili na yenye uwazi. Vituo vya redio vinahimizwa kuweka sera madhubuti za kulinda faragha, usalama wa taarifa na kuhakikisha maamuzi ya kibinadamu yanabaki kuwa msingi wa maudhui. AI ichukuliwe kama nyenzo ya kusaidia ubunifu, si kuchukua nafasi ya sauti ya mwanadamu.

Siku ya Redio Duniani ilitangazwa rasmi mwaka 2011, ikiadhimisha siku ambayo United Nations Radio ilianzishwa mwaka 1946. Redio inaendelea kuwa chombo chenye gharama nafuu, kinachofikia watu wengi zaidi duniani, hususan katika maeneo ya mbali na wakati wa dharura ikiunganisha jamii na kukuza mazungumzo yenye manufaa.

Madelemo news inawatakia wadau wake wote ikiwemo wasikilizaji na wafuatiliaji wa mitandao  ya kijamii kuendelea kuwa nasi kwa kila hatua ikiwa ni sehemu muhimu ya maadhimisho ya siku hii muhimu.

Hakuna maoni: