Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, tarehe 11 Februari 2026.
Kwa mujibu wa utabiri huo:
Katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, pamoja na Dodoma na Singida, kunatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua, huku maeneo machache yakitarajiwa kupata mvua nyepesi zenye ngurumo katika vipindi vifupi.
Kwa upande wa Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, pamoja na Mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi, hali ya hewa inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua, huku mvua za hapa na pale zenye ngurumo zikitarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Katika Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu, kunatarajiwa hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua, pamoja na uwezekano wa mvua za radi katika maeneo machache.
Kwa Visiwa vya Unguja na Pemba, hali ya hewa itakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Aidha, katika Mikoa ya Tanga na Dar es Salaam pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, kunatarajiwa hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua katika kipindi chote cha utabiri.
Kwa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, hali ya hewa inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Vilevile, katika Mkoa wa Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, kutakuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
TMA imewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari pale inapohitajika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni