Breaking


Jumanne, 3 Februari 2026

VIDEO: CRDB YAENDELEZA TEKNOLOJIA KUKUZA UJUMUISHWAJI WA KIFEDHA TANZANIA


Benki ya CRDB imesema itaendelea kutumia teknolojia kubuni bidhaa za kifedha zinazolingana na Dira ya Maendeleo ya 2050, ikiwa ni mkakati wa kuimarisha ujumuishaji wa kifedha, kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wadau wa kiuchumi na kuimarisha ushindani wa Tanzania katika uchumi wa kidijitali wa kikanda na kimataifa.

Akizindua kampeni ya mwaka 2026 ya CRDB "Panga Mkakati Wako" jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, amesema benki imejipanga kutumia ubunifu wa kiteknolojia kuunda suluhu za kifedha zitakazosaidia Serikali kufikia lengo la kuwa na pato la taifa la dola za Marekani trilioni 1.

Nsekela amesema CRDB inaona fursa kubwa katika sekta zinazokua kwa kasi za kidijitali, ikiwemo utengenezaji wa maudhui mtandaoni (content creation), na kwamba benki hiyo inatoa mikopo na huduma maalum za kifedha kwa wabunifu wa maudhui, wajasiriamali wa kidijitali na kampuni za teknolojia ili kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa upande wa utendaji wa kifedha, CRDB imesema ilifunga mwaka 2025 kwa faida ya shilingi trilioni 1.04, ikitoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 13.7, huku mizania ya benki (Balance Sheet) ikikua hadi zaidi ya shilingi trilioni 22, jambo linaloonyesha uimara wa mtaji na imani ya wateja katika benki hiyo.

Hakuna maoni: