Breaking


Jumanne, 3 Februari 2026

VIDEO: SWIFPACK YAONGEZA UFANISI, USALAMA NA URAHISI KWA ABIRIA NA WAFANYABIASHARA


BAADA ya kusimama kwa muda kufuatia mchakato wa maboresho ya kiufundi na kiuendeshaji, huduma ya kidijitali ya usafiri na usafirishaji wa mizigo ya Swifpack, inayomilikiwa na Shirika la Posta Tanzania -TPC, imerejea rasmi, ikiwa na mabadiliko yanayolenga kuimarisha utoaji wa huduma na kukabiliana na mahitaji ya sasa ya watumiaji katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Huduma hiyo imefanyiwa maboresho yanayolenga kuongeza ufanisi wa mfumo, kuimarisha usalama na kurahisisha matumizi kwa abiria, madereva na wafanyabiashara ambapo maboresho hayo yamezingatia changamoto zilizojitokeza hapo awali pamoja na maoni ya watumiaji wa huduma hiyo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam kuhusu kurejea kwa Swifpack, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania,  Ferdinand Kabyemela, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Shirika hilo kuhakikisha linatoa huduma za kidijitali zinazoendana na mahitaji ya soko na mabadiliko ya teknolojia.

Hakuna maoni: