Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kushiriki na kushuhudia hafla ya ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo, tukio lililovutia hisia na hamasa kubwa miongoni mwa wakazi wa jiji hilo.
Soko hilo linafunguliwa rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kukamilika kwa ukarabati wa Soko la zamani la Kariakoo pamoja na ujenzi wa soko jipya la kisasa lenye ghorofa sita (6).
Mradi wa ukarabati na ujenzi wa soko hilo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 28, fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya biashara na kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira salama na ya kisasa.
Ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi, kuimarisha biashara ndogondogo na kubwa, pamoja na kuifanya Kariakoo kuendelea kuwa kitovu kikuu cha biashara nchini.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni