Kwa ujumla, hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Machi 24, 2026, inatarajiwa kuwa ya mawingu yenye mvua na ngurumo katika maeneo machache, huku baadhi ya maeneo yakipata vipindi vya jua.
Aidha, upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya hadi kilomita 30 kwa saa kutoka Kusini Mashariki, na hali ya bahari kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.
Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki dhidi ya mvua hizo, huku matarajio yakionesha kuendelea kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi ifikapo Alhamisi, Machi 26, 2026.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni