Breaking


Ijumaa, 20 Machi 2026

BASATA YAMUONYA MSANII BI HALIMA (SHIKA MAPEMBE) KWA KUKIUKA MAADILI KWENYE VIDEO YA MUZIKI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa onyo kali kwa wasanii nchini kufuatia kusambaa kwa kipande cha video ya muziki kinachodaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania. 

Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa Machi 20, 2026, BASATA imeeleza kuwa tayari imefanya mazungumzo rasmi na msanii Bi. Halima Haji pamoja na meneja wake Rahma R. Pascal, ambapo wote wamekiri kufanya kosa hilo, na sasa taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Katika msisitizo wake, BASATA imewataka wasanii wote kuzingatia mwongozo wa maadili wakati wa kuandaa na kusambaza kazi zao za sanaa ili kulinda utamaduni na heshima ya jamii. 

Baraza hilo limeweka wazi kuwa halitavumilia ukiukwaji wa maadili, na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa msanii yeyote atakayebainika kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti maudhui yasiyofaa katika sekta ya sanaa nchini.

Hakuna maoni: