Breaking


Ijumaa, 20 Machi 2026

MAGORI: UBORA WA LIGI UNATOKANA NA USHINDANI WA KWELI BILA MAIGIZO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Sports Club Crescentius Magori, amesema ubora wa ligi yoyote unatokana na ushindani wa kweli unaojumuisha ushindi, sare na kupoteza bila kuwepo kwa maigizo uwanjani. 

Ameeleza kuwa ni muhimu kwa wadau wa soka kuacha mpira uchezwe kwa haki na uwazi ili kuongeza kiwango na hadhi ya ligi ya Tanzania.

Amesisitiza kuwa nidhamu ya timu na wachezaji ni msingi muhimu katika kujenga ligi yenye mvuto, akibainisha kuwa mashabiki hupata burudani ya kweli pale mchezo unapochezwa kwa kuzingatia sheria na kanuni. 

Aidha, amesema ushindani wa haki huwapa wachezaji nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwa uhuru na kuongeza ubora wa mchezo.


Akizungumzia Simba SC, Magori amesema mechi za timu hiyo zimekuwa kivutio kikubwa kutokana na kucheza kwa kiwango cha juu bila maigizo, jambo linaloifanya kuwa mfano kwa timu nyingine. 

Amehitimisha kwa kusisitiza kuwa endapo timu zote zitafuata misingi hiyo, ligi ya Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa na kuwa miongoni mwa ligi bora barani Afrika.

 

Hakuna maoni: