Breaking


Jumapili, 5 Aprili 2026

ALPHANGA BLACK ALAMBA TUZO KUBWA AFRIKA MASHARIKI

Alphonce  Muyinga maarufu kama Alphanga black, ametunukiwa tuzo ya kiongozi kijana anayechipukia na kuvutia (Emerging and Influential Leader) katika usiku wa tuzo za Afrika Mashariki, uliofanyika nchini Tanzania, mkoani Arusha.


"Tuzo hii ni kwa ajili ya vijana wote katika kanda yetu ya Afrika Mashariki wanaopenda amani, Tuzo hii ni kwa ajili ya vijana wazalendo wanaopenda umoja na mshikamano katika nchi zao na kanda yetu kwa ujumla, Mimi Alphonce Muyinga ni mzalendo, lakini tuzo hii ninaielekeza kwa mzalendo namba moja wa taifa letu, Daktari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema Muyinga baada ya kupokea tuzo hiyo.


Tuzo hizo zilizofanyika jijini Arusha zimeandaliwa na East Africa Youth Awards na kujumuisha nchi zote za kanda ya Afrika Mashariki huku lengo ikiwa ni kutoa motisha kwa vijana katika sekta mbalimbali za uongozi ndani ya Afrika Mashariki.

Hakuna maoni: