Breaking


Ijumaa, 20 Machi 2026

CHUCK NORRIS AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 86

Chuck Norris, gwiji wa filamu za mapigano na nyota maarufu wa Hollywood, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia yake. 

Kifo chake kimeacha simanzi kubwa kwa mashabiki na wadau wa sanaa duniani kote.

Norris alijipatia umaarufu mkubwa kupitia tamthilia ya televisheni Walker, Texas Ranger, pamoja na filamu ya kihistoria ya mapigano The Way of the Dragon, ambapo alionyesha uwezo wake mkubwa wa sanaa za kijeshi dhidi ya Bruce Lee.

Katika taarifa yao, familia ilieleza kuwa Norris aliishi maisha yenye misingi ya imani, nidhamu na upendo kwa watu wake wa karibu. Walisisitiza kuwa alikuwa mtu aliyegusa maisha ya wengi kupitia kazi na tabia yake ya kipekee.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu katika tasnia ya filamu bali pia kwa familia yake ambapo wameeleza kuwa kwao alikuwa zaidi ya nyota wa filamu, alikuwa nguzo ya familia, baba mwenye upendo na mtu aliyewajali sana wapendwa wake. 

Hakuna maoni: