Bank of Tanzania imetoa viwango elekezi vya ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa tarehe 5 Machi 2026, vikionyesha mwenendo wa thamani ya sarafu mbalimbali dhidi ya shilingi ya Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu hizo, dola ya Marekani inanunuliwa kwa Shilingi 2,541.1881 na kuuzwa kwa Shilingi 2,566.6, huku Pauni ya Uingereza ikinunuliwa kwa Shilingi 3,392.4861 na kuuzwa kwa Shilingi 3,426.411.
Kwa upande wa sarafu nyingine, Euro inanunuliwa kwa Shilingi 2,954.8935 na kuuzwa kwa Shilingi 2,984.4425, wakati Yuan ya China inanunuliwa kwa Shilingi 368.4056 na kuuzwa kwa Shilingi 372.0897. Sarafu za ukanda wa Afrika Mashariki pia zimeonesha viwango tofauti ambapo Shilingi ya Kenya inanunuliwa kwa Shilingi 19.6686 na kuuzwa kwa Shilingi 19.8653, huku Shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa Shilingi 0.6877 na kuuzwa kwa Shilingi 0.6946.
Katika taarifa hiyo, BOT pia imeonesha bei elekezi ya dhahabu ambapo wakia moja ya dhahabu inanunuliwa kwa Shilingi 13,119,646.02 na kuuzwa kwa Shilingi 13,250,842.48. Viwango hivi hutolewa kila siku na Benki Kuu kwa ajili ya kutoa mwongozo wa masoko ya fedha na biashara za kimataifa nchini.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni