Tume ya Madini imetangaza bei elekezi za madini kwa tarehe 04 Machi 2026, zikionesha mwenendo wa soko la dunia na bei katika masoko ya ndani. Kwa upande wa dhahabu, bei ya soko la dunia imefikia dola za Marekani 5,217.30 kwa wakia (toz), sawa na Shilingi 429,922.56 kwa gramu.
Bei ya soko la madini hapa nchini imewekwa kuwa Shilingi 386,930.31 kwa gramu, huku bei katika vituo vya ununuzi ikiwa Shilingi 378,331.85 kwa gramu.Kwa upande wa fedha (silver), bei ya soko la dunia ni dola za Marekani 84.47 kwa wakia, sawa na Shilingi 6,960.60 kwa gramu. Bei ya soko la madini imefikia Shilingi 6,264.54 kwa gramu, na bei katika vituo vya ununuzi ni Shilingi 6,125.33 kwa gramu.
Tume imeeleza kuwa bei hizi ni elekezi na zinaweza kubadilika kulingana na mwenendo wa soko la dunia pamoja na hali ya biashara ya madini nchini.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni