Breaking


Jumatatu, 16 Machi 2026

TPSF NDANI YA ONE STOP CENTER YA TISEZA

TPSF na TISEZA wasaini makubaliano ya ushirikiano yatakayorahisisha uwekezaji, kuunganisha wafanyabiashara wa ndani na wawekezaji wa kimataifa

Kupitia makubaliano aya sasa TPSF itakua na uwakilishi ndani ya One stop center TISEZA

Makubaliano hayo yamesainiwa Machi 16, 2026 kati ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPSF, Bw. Deogratius Massawe, na Mkurugenzi Mtendaji wa TISEZA, Bw. Gilead Teri.

Kupitia ushirikiano huo, pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana katika kuhamasisha uwekezaji kwa kutumia majukwaa mbalimbali ya uwekezaji, safari za biashara (trade missions) pamoja na maonesho ya biashara ndani na nje ya nchi.

Ushirikiano huo pia unalenga kuimarisha mawasiliano kati ya sekta binafsi na Serikali, pamoja na kujadili maboresho ya sera, sheria na kanuni ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.

Aidha, katika utekelezaji wa makubaliano hayo, TPSF itaanza kutoa huduma katika One Stop Center ya TISEZA ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa. Hatua hiyo inatarajiwa kusaidia kutoa mwongozo kwa wawekezaji, kurahisisha mawasiliano na taasisi za serikali, na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na uwekezaji katika ukanda.

Hakuna maoni: