Mjadala huo uliwapa fursa wadau wa sekta binafsi kupata ufafanuzi wa kina kutoka TPA kuhusu dhamira, msingi, na umuhimu wa mabadiliko ya tozo zilizotangazwa tarehe 8 Machi 2026. Aidha, TPA iliwasilisha taarifa rasmi ikielezea mantiki ya marekebisho hayo pamoja na matarajio yake katika kuboresha ufanisi wa bandari na huduma za usafirishaji
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, alieleza kuwa Serikali imekuwa sikivu kwa kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, na akaihakikishia sekta binafsi kuwa *TPA si taasisi ya kuwazuia kufanya biashara, bali ni taasisi inayolenga kurahisisha na kuwezesha shughuli za biashara (facilitating institution)* .Aliongeza kuwa maoni yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi mapana ya uchumi wa taifa.
Katika hitimisho la mjadala huo, wadau wote walikubaliana kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufanisi wa bandari za Tanzania ili ziweze kushindana kikanda na kimataifa. Hata hivyo, walisisitiza kuwa mfumo wa tozo unapaswa kuwa stahimilivu kwa biashara (sustainable and business-friendly), na kwamba baadhi ya sekta au biashara zenye hali maalum (special cases) zinapaswa kupewa nafasi ya kuwasilisha athari zake kwa kina ili ziangaliwe kwa umakini zaidi na Serikali
Aidha, Serikali kupitia TPA ilitoa hakikisho kuwa itaendelea kushughulikia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na wadau, na kwamba mrejesho rasmi utatolewa mara baada ya uchambuzi kukamilika kabla ya utekelezaji wa tozo kuanza tarehe 1/07/2026






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni