Matumizi ya Shisha na Sigara yanatajwa kusababisha kwa kiasi kikubwa magonjwa ya Moyo, pamoja na matatizo ya Mapafu na Saratani.
Kutokana na hatari hiyo, vijana na wananchi kwa ujumla wametakiwa kutunza afya zao na kujiepusha na matumizi ya Tumbaku, hususan Sigara na Shisha yanayoweza kupelekea magonjwa ya Moyo, hivyo kusababisha vifo vya ghafla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete-JKCI, Dokta Peter Kisenge, amelezea hatari hiyo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa taarifa ya mwaka 2025 kuhusu kampuni za tumbaku zinavyoingilia Sera ya Afya nchini.
Dokta Kisenge, ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa wa Moyo, amesema matumizi ya tumbaku yanachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha vifo vya gafla vinasababishwa na madhara ya tumbaku katika mishipa ya Moyo ya damu inayosababisha magonjwa ya Moyo.
Matumizi ya tumbaku kwa vijana yanaongezeka ikiwemo uvutaji wa kisasa wa sigara aina ya Shisha, kwani kuvuta Shisha mara moja ni sawa na kuvuta sigara 100, jambo ambalo lina madhara makubwa kwenye mishipa ya damu ya Moyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni