Rais wa Marekani Donald Trump amezungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer kuhusiana na umuhimu wa kuufungua tena Mlango Bahari wa Hormuz, ambao kwa sasa umezuiwa na Iran.
Ofisi ya Waziri Mkuu Starmer, imesema viongozi hao walijadiliana kuhusu hali ilivyo Mashariki ya Kati pamoja na umuhimu kwa kufungua tena Mlango Bahari huo ili kukabiliana na kadhia ya usafirishaji na inayochochea kupanda kwa gharama kote ulimwenguni.
Rais Trump, mapema ametoa rai kwa mataifa mengine kama China na Ufaransa kupeleka Manowari za kivita kuisaidia Uingereza kuufungua mlango huo wa Hormuz.
Aidha, Waziri Mkuu wa Uingereza, Starmer, ametua salamu za pole kwa familia za wanajeshi wa Marekani waliopoteza maisha kwenye vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni