Klabu ya Chelsea inadaiwa kupanga kuharakisha mipango ya kumsajili winga chipukizi wa Ufaransa, Rayane Messi, mwenye umri wa miaka 18, anayekipiga katika klabu ya RC Strasbourg Alsace.
Kwa mujibu wa taarifa za tetesi za usajili barani Ulaya, Chelsea inaangalia uwezekano wa kukamilisha dili hilo mapema ili kuwazidi nguvu vigogo wengine wanaomuwania nyota huyo kijana. Rayane Messi amekuwa akivutia macho ya klabu kadhaa kubwa kutokana na kiwango chake kizuri na uwezo wake wa kucheza kama winga.
Mbali na Chelsea, klabu nyingine kubwa barani Ulaya zinazotajwa kuonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo ni Bayern Munich, FC Barcelona pamoja na Paris Saint-Germain. Ushindani huo unatarajiwa kufanya vita ya usajili kuwa kali katika dirisha lijalo.
Rayane Messi anaonekana kama mmoja wa vipaji vipya vinavyochipukia katika soka la Ulaya, na klabu kadhaa zinaamini anaweza kuwa nyota mkubwa siku zijazo ikiwa ataendelea kukuza kiwango chake uwanjani.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni