Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Noel Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Ahn Eunju, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha na kuendeleza ushirikiano, hususan katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi, biashara na uwekezaji. Wakisisitiza umuhimu wa kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi na kuchochea maendeleo.
Vilevile, pande zote mbili zimeazimia kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kimkakati kwa lengo la kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa yote mawili.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni